Search This Blog

Tuesday, April 21, 2020

Smallinga na Mkhitaryan kuendelea kukipiga AS Roma

Klabu za Man United na Arsenal zimeipa baraka klabu ya AS Roma ya nchini Italia kuendelea kuwa na wachezaji Chris Smalling na Henrikh Mkhitaryan kama walivyoomba.

Smalling yuko AS Roma kwa mkopo akitokea Man United wakati Mkhitaryan akiwa kwa mkopo akitokea Arsenal lakini kusimama kwa Ligi ya Italia kwa sababu ya corona kulisababisha changamoto ya mikataba ya mkopo ya wachezaji hao kuwa itamalizika kabla ya Ligi kuisha.

Hivyo AS Roma ikatuma maombi rasmi katika vilabu vya wachezaji hao kuendelea kuwa nao kwa mkopo hadi June 30, AS Roma wakiamini kuwa janga la corona linawezekana kuwa limeisha na kupungua na Ligi itakuwa imemalizika.

No comments:

Post a Comment

Punguza kilo tano kwa siku saba

  NI watu wachache wanaopenda kunenepa, wengi wanapenda miili ya wastani kwa kuwa  unene si mzuri. Ukiwa mnene si tu kwamba unakaribisha m...