Mshambuliaji wa zamani wa Man City Mario Balotelli ameweka wazi kuwa alikuwa mbioni kujiunga na klabu ya Juventus ya Italia akitokea Man City kabla ya kubadilisha mawazo.
Balotelli aliondoka Man City 2013 baada ya kuitumikia kwa miaka mitatu na kuisaidia kushinda taji la Ligi Kuu England (EPL), amefichua kuwa Juventus ilikuwa ikimuhitaji ajiunge nao.
“Adriano Galliani alinitaka nijiunge na Milan baada ya kuondoka Man City, kama unavyojua mimi ni shabiki wa Milan hivyo nilifuata moyo wangu wakati huo, Milan walikuwa nafasi ya 7 au 8 katika msimamo wa Ligi, hivyo lisingekuwa jambo zuri kwangu kwenda Juventus wakati huo” - Balotelli
Mario Balotelli ,29, ambaye kwa sasa anaichezea Brescia ya Italia, alicheza Man City kwa miaka mitatu 2010-2013 na kujiunga na AC Milan aliyodumu nayo mwaka mmoja tu kabla ya 2014 kuuzwa Liverpool ila akawa na wakati mgumu kiasi cha 2016 kumrudisha Milan kwa mkopo.
Search This Blog
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
Punguza kilo tano kwa siku saba
NI watu wachache wanaopenda kunenepa, wengi wanapenda miili ya wastani kwa kuwa unene si mzuri. Ukiwa mnene si tu kwamba unakaribisha m...
-
Kiwanja kinauzwa kipo Dodoma Mahungu njia ya kwenda Singida kabala hujafika NALA. Kiwanja ni cha Makazi kinaukubwa wa Sqm 450 ( 15 X...
-
Akionekana kwa mara ya kwanza kwa umma tangu aondoke madarakani, aliyekuwa Rais wa Marekani Donald Trump ameweka wazi uwezekano wa kuwania...

No comments:
Post a Comment