Search This Blog

Sunday, April 26, 2020

Kocha Crystal Palace ajiengua kwa corona

London, England. Kocha wa Crystal Palace Roy Hodgson huenda akakosa mechi zote za Ligi Kuu England zilizobaki msimu huu.

Hodgson (72) amepanga kutojitokeza katika mechi kwa kuhofia maambukizi ya virusi vya covid-19.

Kocha huyo wa zamani wa England, amewaambia marafiki zake hatakaa kwenye benchi au kuongoza mazoezi.

Hodgson anahofia kupata maambukizi hayo endapo atajitokeza  katika mkusanyiko.

Timu zimepanga kurejea uwanjani kuendelea na ligi katikati ya mwezi Juni na huenda mechi hizo zikachezwa mbele ya mashabiki wasiozidi 300.

Hodgson amekuwa katika uangalizi maalumu katika kipindi chote tangu janga hilo lilipoibuka.

Advertisement

Let's block ads! (Why?)

No comments:

Post a Comment

Punguza kilo tano kwa siku saba

  NI watu wachache wanaopenda kunenepa, wengi wanapenda miili ya wastani kwa kuwa  unene si mzuri. Ukiwa mnene si tu kwamba unakaribisha m...