
London, England. Manchester United iko tayari kuwapiga bei Paul Pogba ili kupata fedha za kumsajili Jadon Sancho.
Man United inahaha kusaka saini ya winga huyo wa Borussia Dortmund katika usajili wa majira ya kiangazi.
Pogba wanataka kutolewa kafara ili kupata Paini100 inazotaka Dortmund.
Uamuzi huo umefikiwa baada ya mtendaji Ed Woodward kudai klabu hiyo haitatumia fedha nyingi katika usajili wa msimu ujao.
Wachezaji wengine wanaotarajiwa kuwekwa sokoni ni Jesse Lingard, Marcos Rojo na Andreas Pereira.
Woodward ameonya hana bajeti ya usajili mpana kutokaa na mtikisiko wa kiuchumi kutokana na janga la maambukizi ya virusi vya covid-19.
Juventus inataka saini ya Pogba ambaye alicheza kwa kiwango bora kabla ya kurejea Man United.
Kocha wa Man United Ole Gunnar Solskjaer alitumia Pauni47 kumsajili kiungo wa Sporting Lisbon Bruno Fernandes in Januari.
No comments:
Post a Comment