
STAA wa zamani wa Yanga na Taifa Stars, Bakari Malima 'Jembe Ulaya' amesema wachezaji wa sasa endapo watathimini na kujua kwa nini majina ya zamani yanatamba mpaka sasa wataongeza bidii.
Amesema wachezaji wa sasa wapo katika kipindi kizuri ambacho soka lina sayansi na teknolojia, tofauti na enzi zao lakini anaona wanahitaji kuongeza bidii ili kufanya vitu vikubwa.
Amesema wajitahidi kuwa na ushindani na wivu wa maendeleo ya kuhoji wachezaji wa zamani walifanya nini mpaka majina yao yameacha alama.
"Wana roho fulani za kuridhika lakini endapo kama kila siku wangetamani kufanya makubwa basi wengi wao wangekuwa wanacheza nje hivyo timu ya taifa ingekuwa na mabadiliko makubwa,"
"Wapo wale ambao wanapambana kwa kadri wawezavyo kuhakikisha wanafanya vitu vikubwa, ushauri wangu wajitume soka lina mwisho,"amesema.
No comments:
Post a Comment