
MSHAMBULIAJI wa KMC, Salim Aiyee amesema msimu huu ulikuwa na changamoto nyingi ambazo zimeshusha thamani yake.
Amesema mchezaji mzuri ni yule ambaye anatathimini kazi zake kisha anaweka bidii kuhakikisha anafanya makubwa zaidi kwa lengo la kufika mbali.
Amesema anajipanga na kutumia kipindi hiki cha mapumziko kujiweka fiti ili kurejesha makali yake ya kucheka na nyavu.
"Najua ni majeraha ndio yamenifanya niwe na bao moja mpaka sasa, jambo linaloumiza kichwa changu maana kazi yangu ni kucheza na sio vingiu,"
"Uchungu ninaopata wa kumiliki bao moja utanifanya nijitume kwa bidii ili msimu mwingine niweze kurejea kishujaa, napenda kazi yangu naamini nitatimiza ninayoyatamani," amesema.
Msimu ulioisha Aiyee alimaliza na mabao 19 na 'pray off' mawili akiwa na Mwadui FC, ndani ya timu yake ya sasa KMC ana bao moja.
No comments:
Post a Comment