Search This Blog

Sunday, April 19, 2020

Hispania yataka kurefusha hatua za kuzuwia watu kutoka nje

Serikali ya Uhispania inapanga kurefusha hatua ya kuifunga nchi hiyo kwa wiki mbili zaidi baada ya kuona idadi ya vifo kutokana na virusi vya corona ikiongezeka hadi watu 20,043 hadi kufikia jana.

 Ombi la waziri mkuu Pedro sanchez la kurefusha hatu ya kubakia majumbani hadi Mei 9 inalazimika kuidhinishwa na bunge, lakini hatua hiyo inaonekana kuwa na uhakika wa kupita kwa kuwa upinzani umeonesha kuunga mkono.

Sanchez amesema katika hotuba kwamba hatua hiyo ya kurefushwa inahitajika licha ya hatua za maendeleo kupigwa katika udhibiti wa kusambaa kwa maambukizi.

Kwa muda wa wiki tano raia wa Uhispania wapatao milioni 47 waliruhusiwa kutoka majumbani mwao kwa sababu muhimu tu, hususan kwenda kazini , kwa daktari, ama kwenda kununua chakula.

 Tofauti na nchi nyingine, matembezi ya nje na michezo bado hayaruhusiwi.

No comments:

Post a Comment

Punguza kilo tano kwa siku saba

  NI watu wachache wanaopenda kunenepa, wengi wanapenda miili ya wastani kwa kuwa  unene si mzuri. Ukiwa mnene si tu kwamba unakaribisha m...