Search This Blog

Sunday, April 19, 2020

Waliofariki Ulaya kutokana na virusi vya corona wapindukia 100,000

Vifo kutokana na janga la virusi vya corona katika mataifa ya Ulaya yaliyoathirika kwa kiasi kikubwa vimefikia zaidi ya laki moja hadi kufikia jana, wakati nchini Marekani mamia ya waandamanaji wakitiwa nguvu na rais Donald Trump waliandamana dhidi ya amri ya kutotoka nje inayoathiri uchumi wa nchi hiyo.

Wasanii kutoka sehemu mbali mbali duniani walifanya tamasha la muziki lenye nia ya kuwaunga mkono wafanyakazi wa sekta ya afya , na kuleta hali ya umoja wa kijamii katika wakati huu wa mzozo.

Tukio hilo lililochukua muda wa masaa sita mtandaoni lilijumuisha waimbaji kama Billie Eilish na Rolling Stones, lililotayarishwa na kundi la utetezi la Global Citizen pamoja na shirika la afya ulimwenguni WHO.

Duniani kiasi watu 2,281,334 wamepatikana na maambukizi ya virusi vya corona hadi sasa.

Mataifa ya Ulaya yamekabiliwa na vifo vya watu 100,510 , ikiwa karibu theluthi mbili ya watu wote 157,163 waliofariki duniani kote, kwa mujibu wa idadi iliyotolewa na shirika la habari la Ufaransa AFP, wakati karibu robo ya vifo vimetokea nchini Marekani.

Watu 38,000 wamefariki nchini Marekani hadi jana Jumamosi, kwa mujibu wa idadi iliyotolewa na chuo kikuu cha Johns Hopkins.

No comments:

Post a Comment

Punguza kilo tano kwa siku saba

  NI watu wachache wanaopenda kunenepa, wengi wanapenda miili ya wastani kwa kuwa  unene si mzuri. Ukiwa mnene si tu kwamba unakaribisha m...