Search This Blog
Wednesday, April 22, 2020
Dc Kimanta aridhishwa na ujenzi wa nyumba za walimu shule ya Ole Sokoine
Na John Walter- Monduli.
Mkuu wa Wilaya ya Monduli Iddi Kimanta ameitembelea shule ya Sekondari Ole Sokoine iliopo kata ya Monduli juu na kukagua hatua za ujenzi wa nyumba mbili za walimu.
Gharama za ujenzi wa nyumba hizo inatajwa kuwa shilingi milioni mia moja (100) huku wananchi wa Kata za Monduli juu na Mfereji ambao watoto wao wanasoma katika shule hiyo wakiunga mkono hatua hizo ya ujenzi kwa kufanya kazi za mikono kwa kuchimba msingi,kukusanya mawe pamoja na kuchimba mashimo ya vyoo ili walimu waweze kuwa karibu na shule na kuwafanya wanafunzi wafanye vizuri katika masomo yao.
Aidha Kimanta amewapongeza wananchi hao kwa kuunga mkono jitihada hizo za mandeleo.
Katika ziara hiyo Mkuu wa wilaya Iddi Kimanta aliongozana na Mkurugenzi Mtendaji wa wilaya hiyo Stephine Ulaya na Mhandishi wa wilaya Eng. Peter Shemahonge.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
Punguza kilo tano kwa siku saba
NI watu wachache wanaopenda kunenepa, wengi wanapenda miili ya wastani kwa kuwa unene si mzuri. Ukiwa mnene si tu kwamba unakaribisha m...
-
Kiwanja kinauzwa kipo Dodoma Mahungu njia ya kwenda Singida kabala hujafika NALA. Kiwanja ni cha Makazi kinaukubwa wa Sqm 450 ( 15 X...
-
Akionekana kwa mara ya kwanza kwa umma tangu aondoke madarakani, aliyekuwa Rais wa Marekani Donald Trump ameweka wazi uwezekano wa kuwania...

No comments:
Post a Comment