Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa linatarajiwa wiki ijayo kupitisha azimio la kwanza juu ya janga la corona huku miito ikiendelea kutolewa kuhusu kuimarisha ushirikiano wa kimataifa.
Baraza hilo linatarajia kupitisha azimio hilo licha ya mivutano kati ya Marekani, China na Urusi.
Lengo la azimio hilo ni kuunga mkono juhudi za Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres na mashirika kadhaa ya Umoja huo yanayopambana ili kuzuia maakumbizi ya virusi vya corona na athari zake za kisiasa, kiuchumi na kijamii.
Hata hivyo kizingiti kikubwa ni namna ambavyo azimio hilo litawaunganisha kwa kuzingatia wajibu wa shirika la afya duniani, WHO ambalo limelalamikiwa mara kadhaa na rais Donald Trump.
Profesa Bertrand Badie wa chuo cha mitaala ya siasa cha mjini Paris amesisitiza kwamba binadamu bilioni saba na nusu duniani wanahitaji sera ya pamoja kwa sasa kuliko wakati mwingine wowote na ametanabahisha juu ya sera za kutetea maslahi ya kitaifa ambazo amesema zimeongezeka duniani.
No comments:
Post a Comment