Search This Blog

Sunday, April 26, 2020

Idadi ya watu wanougua COVID -19 yapungua kidogo Ujerumani


Idadi ya watu wanaougua COVID-19 hapa nchini Ujerumani imepungua kwa kiwango kidogo, huku Taasisi ya Robert Koch ikisema kuna maambukizi mapya 1737 yaliyoorodheshwa leo Jumapili.

Zaidi ya watu 154,000 wameambukizwa virusi hivyo, na idadi ya waliokufa mpaka sasa ikifikia 5640. Taasisi hiyo imesema inakadiria kiwango cha asilimia 0.9 ya maambukizi mapya yatatokea nchini humu.

Wakati huo huo benki ya Co- operative ya Ujerumani DZ, imesema kutokana na janga la corona, karibu robo ya kampuni za Ulaya zitaorodhesha hasara katika mwaka huu.

Benki hiyo imesema kufikia sasa, kampuni 141 kati ya 600 zimetangaza kuwa zitakata gawio kwa mwaka wa fedha uliopita kwenye faharasi ya hisa ya Ulaya ya Stoxx, na malipo yanayotarajiwa kwa mwaka wa fedha wa 2019 yatashuka kwa asilimia 23.


No comments:

Post a Comment

Punguza kilo tano kwa siku saba

  NI watu wachache wanaopenda kunenepa, wengi wanapenda miili ya wastani kwa kuwa  unene si mzuri. Ukiwa mnene si tu kwamba unakaribisha m...