
London, England. Newcastle United imepanga kuzungumza na Napoli kuhusu usajili wa Kalidou Koulibaly majira ya kiangazi msimu ujao.
Wamiliki wapya wa Newcastle wanataka kuisuka upya na tayari wameanza kunyemelea saini za wachezaji nyota Ulaya.
Mshambuliaji nguli wa Paris Saint Germain (PSG) Edinson Cavani na Nabil Fekir wapo katika rada za klabu hiyo ya St James Park.
Koulibaly amekuwa akihusishwa na Manchester United ambayo inapewa nafasi baada ya Napoli kumuweka sokoni.
Mmiliki wa Napoli Aurelio De Laurentiis yuko tayari kumpiga bei beki huyo wa kimataifa wa Senegal.
Newcastle ambayo kwa muda mrefu imekuwa katika mazingira magumu ya kiuchumi, imetuma maombi ya usajili wa beki huyo wa kati pia Cavani na Fekir.
Napoli inataka Pauni70 milioni kwa klabu inayotaka huduma ya Koulibaly. Msimu huu beki huyo hakucheza katika ubora wake kutokana na kuandamwa na majeraha.
No comments:
Post a Comment