Search This Blog
Monday, March 9, 2020
Waziri mkuu wa Sudan arejea ofisini baada ya jaribio la kumuua
Waziri Mkuu wa Sudan, Abdullah Hamdok amerejea ofisini leo mchana, saa chache baada ya jaribio la kumuua kushindwa kwenye mji mkuu wa nchi hiyo, Khartoum.
Msemaji wa baraza la mawaziri, Faisal Mohamed Salih amesema kiongozi huyo anaendelea na majukumu yake ofisini kama kawaida.
Hamdok ameandika katika ukurasa wake wa Twitter kwamba anawahakikishia watu wa Sudan kuwa yuko salama kabisa.
Amesema shambulizi hilo halitorudisha nyuma harakati za Sudan kuelekea katika demokrasia. Faisal amesema vikosi vya usalama vinawatafuta magaidi walioushambulia msafara wa Hamdok.
Shambulizi hilo lilitokea karibu ya gari la kiongozi huyo wakati msafara wale ukipita kuingia kwenye daraja la Kober, kaskazini mwa Khartoum akiwa anaelekea ofisini kwake.
Hakuna kundi lolote ambalo limedai kuhusika na shambulizi hilo.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
Punguza kilo tano kwa siku saba
NI watu wachache wanaopenda kunenepa, wengi wanapenda miili ya wastani kwa kuwa unene si mzuri. Ukiwa mnene si tu kwamba unakaribisha m...
-
Kiwanja kinauzwa kipo Dodoma Mahungu njia ya kwenda Singida kabala hujafika NALA. Kiwanja ni cha Makazi kinaukubwa wa Sqm 450 ( 15 X...
-
Akionekana kwa mara ya kwanza kwa umma tangu aondoke madarakani, aliyekuwa Rais wa Marekani Donald Trump ameweka wazi uwezekano wa kuwania...

No comments:
Post a Comment