Search This Blog

Monday, March 9, 2020

Hukumu ya Mbowe na viongozi wengine wa CHADEMA leo

Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu leo March 10, 2020 inatarajia kutoa hukumu kwa Viongozi wa CHADEMA, wanaokabiliwa na kesi ya uchochezi Mahakamani hapo.

Viongozi wanaokabiliwa na shauri hilo ni pamoja na Mwenyekiti wa CHADEMA, Freeman Mbowe, na Wabunge John Mnyika, Halima Mdee, Ester Bulaya, Ester Matiko, John Heche, Peter Msigwa na pia aliyekuwa Katibu Mkuu CHADEMA kabla ya kuhamia CCM, Vicent Mashinji.

Hukumu hiyo inakuja baada ya February 24, 2020 Hakimu Mkazi Mkuu Thomas Simba kusikiliza ushahidi wa upande wa mashtaka na ule wa utetezi na kutoa siku tano za kazi kwa Mawakili wa pande zote mbili kuwasilisha hoja za majumuisho kwenye shauri .

Washtakiwa wote kwenye shauri hilo namba 112 la mwaka 2018 wanakabiliwa na mashtaka 13 yakiwemo kufanya kusanyiko na maandamano kinyume cha sheria na kutoa maneno ya uchochezi.

No comments:

Post a Comment

Punguza kilo tano kwa siku saba

  NI watu wachache wanaopenda kunenepa, wengi wanapenda miili ya wastani kwa kuwa  unene si mzuri. Ukiwa mnene si tu kwamba unakaribisha m...