KATIKA Kuhakikisha wanafikia malengo, Kocha Mkuu wa Simba, Sven Vandenbroeck amesema wamejipanga kuhakikisha wanapata ushindi katika mechi dhidi ya Azam FC itakayochezwa leo kwenye Uwanja wa Taifa.
Simba wanaongoza Ligi Kuu Tanzania Bara wakiwa na alama 65 baada ya mechi 25, wamepania kuhakikisha mchezo dhidi ya Azam unakuwa ni maandalizi kwa ajili ya kukabiliana na mahasimu wao Yanga hapo Jumapili wiki hii.
Akizungumza na Nipashe jijini jana, Sven alisema anatambua mchezo utakuwa mgumu, lakini anaamini matokeo ya ushindi katika michezo mitano iliyopita ni ishara nzuri katika mchezo huo kupata alama tatu.
Alisema yuko makini kukisuka kikosi chake kuhakikisha kila wanapomaliza mchezo wanakuwa na maandalizi ya mchezo unaofuata.
"Kila kitu ni hatua na kwa sasa tulipo si sehemu mbaya, tunahitaji kuona tunapata matokeo mazuri yatakayotufanya tuzidi kuwa imara," alisema kocha huyo.
Alisema malengo yao ni kufanya vizuri katika michezo iliyopo mbele yao ikiwamo huu wa Azam ambao ni mazoezi tosha kuelekea mechi dhidi ya Yanga.
Alisema kwa sasa hawadharau timu yoyote wanayokutana nayo kutokana na kuhitaji kufanya vizuri na kupata pointi kila mechi kwa michezo iliyobaki.
Naye nahodha wa Simba, John Bocco alisema kuvuna pointi tatu katika kila mchezo kati ya mitano iliyopita kunawapa hamasa ya kutafuta alama zingine katika mechi dhidi ya Azam ambayo itakuwa maandalizi mazuri kwa ajili ya pambano dhidi ya Yanga.
"Wachezaji tumejiwekea mikakati ya kutafuta alama tatu, hivyo KMC ilikuwa ni maandalizi ya mchezo wetu dhidi ya Azam, tunahitaji kupata pointi ili tufikie malengo yetu ya kutwaa taji la ubingwa mara tatu," alisema Bocco.
Lakini Meneja wa klabu hiyo, Patrick Rweyemamu alisema: "Tupo vizuri kukutana na Azam wachezaji wana morali kuhakikisha wanatoka na ushindi na kupeleka maangamizi hayo Jumapili.
"Tunaiheshimu Azam ni timu nzuri tumejipanga kuhakikisha hatuwapi nafasi ya kuliona goli letu kirahisi."
Kwa upande wa Azam FC walisema, jana walifanya mazoezi ya mwisho huku kila mchezaji akiwaza ushindi katika mchezo huo.
Search This Blog
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
Punguza kilo tano kwa siku saba
NI watu wachache wanaopenda kunenepa, wengi wanapenda miili ya wastani kwa kuwa unene si mzuri. Ukiwa mnene si tu kwamba unakaribisha m...
-
Kiwanja kinauzwa kipo Dodoma Mahungu njia ya kwenda Singida kabala hujafika NALA. Kiwanja ni cha Makazi kinaukubwa wa Sqm 450 ( 15 X...
-
Akionekana kwa mara ya kwanza kwa umma tangu aondoke madarakani, aliyekuwa Rais wa Marekani Donald Trump ameweka wazi uwezekano wa kuwania...

No comments:
Post a Comment