Search This Blog
Tuesday, March 3, 2020
Ujenzi wa barabara ya Dodoma- Morogoro kukamilika leo
Waziri wa Ujenzi , Uchukuzi na Mawasiliano Mhandisi Isack Kamwelwe amesema daraja la Mto Mkange lililopo Wilayani Kilosa lililovunjilka Machi 2 mwaka huu, linatarajiwa kukamilika usiku wa kuamkia Machi 4 mwaka huu.
Waziri Kamwelwe amesema hayo akiwa katika eneo la tukio, mara baada ya Karavati moja kati ya mawili yanayohitajika kushushwa sehemum lilipokatika daraja na kutoa matumaini kuwa ujenzi wa daraja hilo la muda utakamilika usiku wa kuamkia Machi 4 Mwaka huu.
Hata hivyo Waziri amesema kuwa daraja hilo kwa sasa halitapitisha magari mawili kwa pamoja badala yake gari moja tu litaruhusiwa kupita hadi hapo utaratibu mwingine utatakapotolewa.
Aidha, Waziri amesema karavati la awali ambalo limevunjika lilikuwa na kipenyo cha Mita tatu tu na sasa yamewekwa makaravati mawili kila moja likiwa na kipenyo cha Mita tatu hivyo kuruhusu maji mengi kupita kwa wakati mmoja tofauti na awali.
Akitoa matumaini kwa watanzania hususana madereva wanaotumia barabara hiyo ya Morogoro – Dodoma, Waziri amesema kazi ya kujenga daraja la kudumu katika eneo hilo utafanyika mara baada ya mvua kupungua.
Kwa upande waka Mkuu wa Mkoa wa Morogoro Loata Ole Sanare amewashukuru wananchi kwa ushirikiano mkubwa waliouonesha tangu adha hiyo ilipotokea hususan madereva kwa kutii maelekezo ya Serikali walipotakiwa kubaki maeneo waliyokuwapo hadi watakapoelekezwa vingine.
Daraja la Mto Mkange lililopo katika Kijiji cha Kiegeya Wilayani Kilosa lilivunjika Machi 2 Mwaka huu majira ya saa kumi jioni kutokana na mvua kubwa zinazoendelea kunyesha hapa nchini na kusababisha adha kubwa kwa wasafiri na Usafirishaji.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
Punguza kilo tano kwa siku saba
NI watu wachache wanaopenda kunenepa, wengi wanapenda miili ya wastani kwa kuwa unene si mzuri. Ukiwa mnene si tu kwamba unakaribisha m...
-
Kiwanja kinauzwa kipo Dodoma Mahungu njia ya kwenda Singida kabala hujafika NALA. Kiwanja ni cha Makazi kinaukubwa wa Sqm 450 ( 15 X...
-
Akionekana kwa mara ya kwanza kwa umma tangu aondoke madarakani, aliyekuwa Rais wa Marekani Donald Trump ameweka wazi uwezekano wa kuwania...

No comments:
Post a Comment