
London, England. Jurgen Klopp amesema matokeo ya jana usiku iliyopata Liverpool dhidi ya Chelsea hayajamuumiza.
Kocha huyo alisema alipata maumivu baada ya kupoteza mechi ya Ligi Kuu dhidi ya Watford.
Kauli ya Klopp imekuja baada ya Liverpool kufungwa mabao 2-0 na Chelsea katika mchezo wa Kombe la FA.
Mabao ya Ross Barkley na Willian yalitosha kuendeleza kipigo kwa timu hiyo katika mechi tatu kati ya nne za mwisho ilizocheza hivi karibuni.
Awali, ilipoteza kwa kufungwa na Atletico Madrid katika mechi ya kwanza ya Ligi ya Mabingwa Ulaya, ilifungwa na Watford kabla ya jana kulala dhidi ya Chelsea.
Liverpool ikiwa ugenini kwenye Uwanja wa Metropolitano timu hiyo ilifungwa bao kabla ya kuchapwa 2-0 dhidi ya Watford.
Klopp alisema kati ya mechi hizo tatu, aliumizwa zaidi na kipigo cha Watford.
“Sina hofu na kiwango cha wachezaji wangu walichoonyesha katika mechi hizi tatu tulizopoteza. Usiku wa leo (jana) hatukuwa katika ubora wetu
“Siwezi kusema mechi hizi zilikuwa nyepesi, hapana zilikuwa ngumu na tulipambana kupata ushindi, lakini lazima tukubali matokeo,”alisema Klopp.
No comments:
Post a Comment