MSHAMBULIAJI wa Simba Queens,Mwanahamisi Omary amesema ukaribu wake na Meddie Kagere na Haruna Niyonzima umemfanya kujifunza ufundi kutoka kwao.
Amesema Kagere amekuwa akimshauri kufanya kazi zake bila kuangalia watu wanasema nini kwake huku akimsisitiza kuyafanya mazoezi yawe sehemu ya maisha yake.
"Najifunza mengi kwa Kagere,jamaa ana juhudi binafsi,huwa ananiambiaga umechagua soka kuwa kazi yako litendee haki,kuwa mwanamke wa mfano wa kuigwa wa maendeleo," amesema.
Mwanahamisi amesema Kagere hajaishia kumwambia bali alimpa njumu mpya kama motisha ya kujituma.
Kwa upande wa Haruna Niyonzima wa Yanga, alisema amekuwa akimshauri namna yakuwa mwanasoka bora wa kike.
"Niyonzima ana roho ya kitofauti amewahi kunisaidia pesa kuna kipindi niliumwa,ukiachana na hilo anapenda bidii yangu kwenye soka, Hilo linanipa somo la kujifunza ufundi wao,"amesema.
Search This Blog
Saturday, March 28, 2020
Kagere, Niyonzima wampa maujuzi Gaucho
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
Punguza kilo tano kwa siku saba
NI watu wachache wanaopenda kunenepa, wengi wanapenda miili ya wastani kwa kuwa unene si mzuri. Ukiwa mnene si tu kwamba unakaribisha m...
-
Kiwanja kinauzwa kipo Dodoma Mahungu njia ya kwenda Singida kabala hujafika NALA. Kiwanja ni cha Makazi kinaukubwa wa Sqm 450 ( 15 X...
-
Akionekana kwa mara ya kwanza kwa umma tangu aondoke madarakani, aliyekuwa Rais wa Marekani Donald Trump ameweka wazi uwezekano wa kuwania...
No comments:
Post a Comment