Search This Blog

Saturday, March 28, 2020

Mastaa hawa ghafla wamepoteza ramani

By Olipa Assa

MASTAA wa Ulaya wana vitu vya msingi wanavyoviangalia kabla ya kufanya uhamisho wa kutoka sehemu moja kwenda nyingine ikiwemo nafasi ya kucheza ili kulinda thamani zao.

Ndio maana utasikia thamani ya mchezaji fulani ni kubwa kipesa inatokana na uwezo ambao wanakuwa wameuonyesha.

Pia wanaangalia dau la usajili ambao linakuwa linatokana na kiwango ndio maana huwezi kusikia Cristiano Ronaldo anasaini timu mpya kisha aende akakae benchi.

Kibongo Bongo kitu kinachoangaliwa ni mkwanja bila kujali nafasi zao kwa timu wanazohamia, hilo limekuwa likiwapoteza wengi kwenye ramani.

Mwanaspoti limefanya utafiti wa wachezaji ambao walikuwa wanaanza vikosi vya kwanza baada ya kuhamia timu nyingine wamepotea kwenye ramani.

IBRAHIM AJIBU

Advertisement

Ajibu kurejea Simba kwa mara nyingine akitokea Yanga ambako alikuwa anapata nafasi katika kikosi cha kwanza cha Kocha Mwinyi Zahera ni kama kumemwondoa kwenye ramani ya kiwango.

Anasugua benchi pale Msimbazi akishuhudia wenzake wakifanya kazi, tofauti na moto wa msimu ulioisha uliofanya saini yake ionekane muhimu.

BENO KAKOLANYA

Kabla ya sintofahamu baina yake na viongozi wa Yanga iliomfanya akae nje ya kazi, alikuwa anadaka kikosi cha kwanza, akimuweka Kindoki na Ramadhan Kabwili.

Alitegemewa kwenda kula mfupa mbele ya Aishi Manula ambao uliwashinda Said Mohamed ‘Nduda’ ambaye yupo Mtibwa Sugar na Deo Munishi ‘Dida’ wa Lipuli.

Beno siku za mwanzo alionekana kupambana ila kadri siku zinavyoendelea anaonekana kukalishwa benchi na Manula.

GADIEL MICHAEL

Usajili wa Gadiel Michael ulitikisa akitokea Yanga ambako alikuwa panga pangua, hata baada ya kusaini Simba mashabiki walikuwa hawawapatii picha ushindani wao na Mohammed Hussein ‘Tshabalala’.

Tshabalala anaonekana kumpiku Gadiel kwani ndiye anaaminiwa kikosi cha kwanza.

ADEYUM SALEH

Alikuwa anaanza kikosi cha kwanza cha JKT Tanzania baada ya kutua Yanga kwa anasubiri namba mbele ya Jafary Mohamed ambaye amekuwa akiaminiwa tangu enzi za Kocha Charles Mkwasa kisha kocha wa sasa Luc Eymael.

SALIM AIYEE

Hakuna asiyejua moto aliyokuwa nao Salim Aiyee wakati yupo Mwadui FC, alimaliza na mabao 19 nyuma ya Meddie Kagere ambaye alimaliza na 23 msimu ulioisha.

Pia aliibakiza timu yake akifunga mabao mawili ya play off, Hilo lilifanya timu kutokwa na udenda wa kuhitaji saini yake,tangu afike KMC amekuwa akisugua benchi na mpaka sasa anamiliki bao moja tu.

IDD SELEMAN ‘NADO’

Nyota yake ilianza kung’ara kwenye ndondo cup kisha akawa msaada mkubwa ndani ya timu ya Mbeya City ambapo msimu wake wa mwisho alimaliza na mabao 10.

Aliweza kuanza kikosi cha kwanza baada ya kusajiliwa Azam FC mpaka akawa anajumuishwa Taifa Stars ila kwa amekuwa haanzi.

Alikuwa pangua Mbeya City, msimu wa mwisho ndani ya timu hiyo alimaliza mabao 10.

ABALKASSIM KHAMIS

Wakati yupo Kagera Sugar,msimu uliopita alimaliza na mabao sita, matajiri wa Azam FC wakavutiwa na huduma yake wakamjumuisha kwenye kikosi chao cha mwaka huu.

Chini ya kocha Mecky Maxime alikuwa panga pangua kwenye kikosi chake cha kwanza, lakini tangu afike Azam FC, anazoea benchi na kushindwa kufurukuta mbele ya straika Obrey Chirwa.

Alikuwa kati ya mabeki ambao walikuwa panga pangua katika kikosi cha kwanza cha KMC, Hilo ndilo lililowavuta Yanga kumsajili wakiamini huduma yake itawafaa.

Ajabu baada ya kutua Yanga, Ali Ali hasikikii kabisa hasa kwenye kikosi cha Luc ambapo anatumtumia zaidi Jafary Mohamed.

HARUNA SHAMTE

Alikuwa moto wa kuotea mbali wakati yupo Lipuli ya Iringa chini ya Kocha Seleman Matola, baada ya kutua Simba, wadau wa soka angempa ushindani Shomary Kapombe, lakini amekalishwa na kusugua benchi.

ALI MTONI ‘SONSO’

Ingawa anapata nafasi Yanga lakini sio kama alivyokuwa Lipuli ambako alikuwa muhimu kwenye kikosi cha kwanza.

Let's block ads! (Why?)

No comments:

Post a Comment

Punguza kilo tano kwa siku saba

  NI watu wachache wanaopenda kunenepa, wengi wanapenda miili ya wastani kwa kuwa  unene si mzuri. Ukiwa mnene si tu kwamba unakaribisha m...