
KIPA wa Polisi Tanzania, Peter Manyika Jr amesema licha ya kusimama kwa ligi kutokana na kuepuka maambukizi ya ugonjwa wa corona, anapata msaada wa baba yake mzazi unaomsaidia kulinda kiwango.
Baba wa mchezaji huyo, Manyika Peter Sr ni kocha wa makipa wa timu ya Yanga,amekuwa akimpa mazoezi mwanae kuhakikisha kiwango chake hakishuki.
Manyika Jr ameliambia Mwanaspoti kwamba baba yake anamsimamia mazoezi na kumshauri namna ya kukuza kiwango chake.
"Msaada wa baba umekuwa mkubwa,licha ya kunisimamia kwa baadhi ya mazoezi bado kuna programu alizonipa zakufanya binafsi,"
"Nimebahatika kuwa na baba ambaye anafuatilia hatua zangu moja baada ya nyingine kuhakikisha sirudi nyuma kwenye kazi zangu,"amesema.
Tangu ajiunge na timu hiyo akitokea nchini Kenya ambako alikuwa anacheza klabu ya KCB, amedaka mechi tatu dhidi ya Singida United, Ndanda na Mwadui ambapo aliweza kuokoa hatari mbili.
No comments:
Post a Comment