Search This Blog
Thursday, March 26, 2020
Jeshi la Ufaransa latangaza kuondoka nchini Irak
Kikosi cha eshi la Ufaransa kilichokuwa nchini Irak katika jeshi la ushirika dhidi ya kundi la Daesh charejea nyumbani.
Jeshi la Ufaransa limetangaza kuondoka nchini Irak kwa kikosi chake kilichokuwa katika jeshi la ushiriki katika mapambano dhidi ya kundi lla kigaidi la Daesh nchini humo.
Kulingana na jeshi la Ufaransa, wanajeshi wake nchini humo Irak wanaondoka kutokana na janga la virusi vya corona.
Taarifa kuhusu jeshi la Ufaransa kuondoka nchini Irak imetolea Jumatano Machi 25.
Kwa ushirikiano na jeshi la Irak, jeshi la ushirikiano limechukuwa uamuzi wa kusitisha kwa muda zoezzi la kutoa mafunzo kwa wanajeshi wa Irak katika juhudi za kupamban na kundi la kigaidi la Daesh.
Jeshi la Ufaransa limefahmisha kuwa limechukua uamuzi huo kutokana na janga la virusi vya corona, virusi ambavyo ni tishia katika pembe nne za dunia.
Wanajeshi zaidi ya 100 wa Ufaransa, kundi la kwanza litaondoka nchini humo Machi 26.
Operesheni za anga za jeshi la Ufaransa dhidi ya kundi la Daesh zitaendelea kutokea katika kambi yake iliopo nchini Yordania.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
Punguza kilo tano kwa siku saba
NI watu wachache wanaopenda kunenepa, wengi wanapenda miili ya wastani kwa kuwa unene si mzuri. Ukiwa mnene si tu kwamba unakaribisha m...
-
Kiwanja kinauzwa kipo Dodoma Mahungu njia ya kwenda Singida kabala hujafika NALA. Kiwanja ni cha Makazi kinaukubwa wa Sqm 450 ( 15 X...
-
Akionekana kwa mara ya kwanza kwa umma tangu aondoke madarakani, aliyekuwa Rais wa Marekani Donald Trump ameweka wazi uwezekano wa kuwania...

No comments:
Post a Comment