Search This Blog

Thursday, March 19, 2020

China haikuripoti visa vipya vya corona kwa siku ya pili

Kwa siku ya pili China haikuripoti visa vipya vinavyotokana na virusi vya corona, isipokuwa maambukizi yanayotoka nje ya nchi hiyo.Kupungua kwa maambukizi mapya nchini humo kunatoa matumaini kwa dunia nzima.

Mataifa mbalimbali ulimwenguni kote yamekuwa yakisitisha shughuli zake za kawaida na kuzuia watu wabakie majumbani katika juhudi za kupunguza kasi ya maambukizi ya virusi hivyo.Virusi hivyo vya corona vinaaminika kuwa vilianzia katika soko la mji wa China wa Wuhan mnamo mwezi Desemba mwaka uliopita.

Watu wapatao milioni 56 katika mji huo wa Wuhan na jimbo jirani la Hubei walilazimika kubakia majumbani tangu mwishoni mwa mwezi Januari mwaka huu.

Hata hivyo China ina wasiwasi wa kuzuka wimbi lengine la maambukizi yanayotoka nje ya nchi. Leo hii, wizara ya afya imeripoti visa 39 zaidi vilivyoingia nchini na kuifanya idadi jumla kufikia visa 228.

No comments:

Post a Comment

Punguza kilo tano kwa siku saba

  NI watu wachache wanaopenda kunenepa, wengi wanapenda miili ya wastani kwa kuwa  unene si mzuri. Ukiwa mnene si tu kwamba unakaribisha m...