Search This Blog

Thursday, March 19, 2020

Siku 7 ngumu kwa wachezaji wa Simba

WACHEZAJI na benchi la ufundi la Simba wamepewa mapumziko ya siku saba tu kutokana na janga la virusi vya corona lakini ndani ya muda huo wanatakiwa kujikinga kwa umakini mkubwa, mazoezi yaendelee kama kawaida na akili ziwaze ubingwa tu.

Uongozi wa Simba kupitia Ofisa Mtendaji Mkuu, Senzo Mazingisa uliwapatia taarifa hiyo wachezaji juzi Jumatano jioni baada ya kufanya kikao akiwa na baadhi ya Wajumbe wa Bodi ya Wakurugenzi pamoja na benchi la ufundi ambalo liliongozwa na Kocha Sven Vandernbroeck.

Moja kati ya masharti ambayo wachezaji wamepewa ni kuhakikisha wanafanya mazoezi binafsi kwa kila mmoja na programu yake aliyopangiwa na mwalimu kutokana na mahitaji na hakuna kufanya starehe ambazo zinaweza kuwathiri viwango na kuwatoa katika mstari wa mbio za ubingwa.

Wachezaji hao wamepewa mbinu mbalimbali za kuhakikisha kwamba wanakuwa salama na familia zao lakini kila walipo wametakiwa kuwaza na kuweka kwenye akili zao kuwa kipaumbele cha Simba ni ubingwa tu ulioko katika mechi tano zilizoko mbele yao, hivyo kila mmoja ajiongeze zaidi.

Mwenyekiti Msaidizi wa Bodi ya Wakurugenzi Simba, Salim Abdallah ‘Try Again’ alisema mapumziko hayo ambayo wamepatiwa wachezaji pamoja na benchi la ufundi yanaweza kugusa maeneo mbalimbali ambayo yatakuwa ni vyanzo vya hasara katika klabu.

“Moja ya chanzo cha kipato ambacho klabu ni kutoka kwa mashabiki wake kuingia viwanjani, kununua jezi na baadhi ya vitu vya klabu ambavyo kwa wakati huu haviwezi tena kupatikana kutokana kila mmoja anajikinga na ugonjwa huu wa corona,” alisema.

Advertisement

“Unajua hawa wachezaji na makocha ni waajiriwa wa klabu na kazi yao ni kucheza mpira ili waweze kulipwa kwa maana hiyo tutawalipa mishahara ya miezi miwili bila ya kufanya kazi ambayo wameajiriwa nayo kwa maana hiyo timu hapa itaingia katika hasara.

“Kipindi kama hiki ligi ikiwa imesimama timu inaingia hasara ya kuwapa tiketi za ndege kwenda na kurudi kwa wachezaji ambao wanatoka nje ya nchi na wale ambao wanaishi nje ya Dar es Salaam, jambo ambalo lingetakiwa kufanyika mara baada ya msimu kumalizika.

“Hawa wachezaji wetu wa kigeni wanaishi katika nyumba ambazo kipindi kama wakiwa hawapo gharama za kuwalipia hapo hazitakuwepo lakini sasa hivi wapo wanaishi bila ya kufanya kazi ambayo imewaleta huku tukiendelea kuwalipia mahitaji yote hayo,” alisema Abdallah.

“Wachezaji na makocha kipindi kama hiki wanaweza kuumwa, kwa lugha rahisi klabu inatakiwa kuingia gharama ya kuwahudumia kwa maana hiyo kuna hasara nyingi ambazo tunaweza kuzipata ila yote kwa yote afya ni bora kuliko mambo mengine yote ndio maana tumewapa mapumziko na tahadhari kubwa wanatakiwa kuichukua wachezaji wetu wote katika kipindi hiki cha ugonjwa hatari wa corona,” alisisitiza Abdallah.

Let's block ads! (Why?)

No comments:

Post a Comment

Punguza kilo tano kwa siku saba

  NI watu wachache wanaopenda kunenepa, wengi wanapenda miili ya wastani kwa kuwa  unene si mzuri. Ukiwa mnene si tu kwamba unakaribisha m...