Mkuu wa Mkoa wa Mara Mhe. Adam Malima ameipongeza Bodi ya Kahawa kwa kutimiza ahadi yake ya kuupa mkoa wake miche bora ya kahawa aina ya arabika mbapo jumla ya miche 40,000 imekabidhiwa katika hafla fupi iliyofanyika leo, tarehe 10 Machi, 2020 katika Ofisi ya Mkuu wa mkoa wa Mara, Mjini Musoma.
Akiongea wakati wa hafla hiyo, Mhe. Adam Malima amesema Bodi ya Kahawa imeonyesha kwa vitendo dhamira yake kama msimamizi wa sekta ndogo ya zao la kahawa kwa kutoa miche 40,000 bora ambayo itasambazwa katika wilaya za mkoa wa Mara ili kuwapa bure, Wakulima ambao wengi wamejiandaa kuipokea na kuipanda.
Mhe. Malima amesema azimo la kuongeza uzalishaji na tija lilifikiwa na Wadau wa zao la kahawa, katika mkutano wa Kamati Ndogo, uliofanyika Mjini Moshi na kukubaliana kuwa katika kipindi cha miaka mitatu, Wizara ya Kilimo kupitia Bodi ya Kahawa kuanza mapinduzi ya kuongeza tija na uzalishaji wa kahawa kutoka tani 50,000 za sasa hadi tani 200,000 ifikapo mwaka 2023.
“Kwenye mkutano wetu wa kamati ndogo ya kahawa, tuliokutana Mjini Moshi, mwezi mmoja uliopita, tulikubaliana kwa pamoja kuongeza uzalishaji na sioni sababu kwa nini tusiizidi nchi ya Uganda ambayo ina eneo dogo lakini inazalisha zaidi ya tani 295,000.” Amekaririwa Mkuu wa mkoa wa Mara.
Mhe Malima amesema Serikali ya mkoa imewaanda Wakulima wake na tayari vitalu vimeandaliwa ili kuhakikisha kuwa Wakulima katika wilaya ya Tarime na wilaya zote za mkoa, wanaongeza uzalishaji kwa kupanda miche hiyo.
“Tumeshaanda mkakati wa mkoa, tumegawana majukumu na niseme tu kuwa Tarime inafanya vizuri na inaongoza ukilinganisha na wilaya ya Butiama, Serengeti na Rolya; tumeshaanzisha vitalu katika wilaya hizo, bila shaka tutaongeza uzalishaji kutoka 15,000 kimkoa za sasa na kufanya vizuri zaidi”. Amesisitiza Mhe Malima.
Akiongea baada ya kukabidhi miche hiyo, Kaimu Mkurugenzi Bodi ya Kahawa, Profesa Jamal Adam amemshukuru Mkuu wa mkoa wa Mara kwa namna ambavyo amedhamilia kuongeza tija na uzalishaji kwenye mkoa wa Mara na ameahidi kuwa Bodi ya Kahawa itaongeza miche 60,000 zaidi ambayo, itapandwa kwenye shamba kubwa la Jeshi la Magereza, Mjini Tarime.
Profesa Jamal Adam ameongeza kuwa Bodi ya Kahawa imeanzisha mkakati wa pamoja wa kuongeza eneo la kilimo cha kahawa kwa kuwahamasisha Wakuu wa mikoa inayolima kahawa na kwa kuanzia uhamasishaji unalenga kila mkoa wilaya inayolima kahawa kuanzisha mashamba mashamba mawili makubwa ya kahawa na kwa kufanya hivyo, uzalishaji utaongezeka katika kipindi kifupi.
“Tuna mashamba makubwa 101 nchini kote, tumekubaliana ili kuongeza uzalishaji wa sasa ambao ni tani 50,000 ni kwa kila wilaya kuanzisha mashamba mawili makubwa ambapo Bodi ya Kahawa, Taasisi ya Utafiti wa Kahawa (TACRI) zitashirikiana na Serikali za mikoa kuhakikisha mashamba hayo yanakuwa endelevu, kwa kufanya hiyo tutafikia uzalishaji wa tani 200,000 katika kipindi kifupi”. Amesisitiza Pro.Adam.
Kaimu Mkurugenzi Bodi ya Kahawa ameongeza kuwa Bodi ya Kahawa itaanzisha mkakati wa kuhamasisha kilimo cha kahawa kuanzia kwenye shule za msingi na sekondari na kwa kufanya hiyo, watoto watajengewa mazingira ya kuanza kulipenda zao la kahawa tangu wakiwa wadogo.
“Tumeanda mkakati wa kuhamasisha kilimo cha zao la kahawa kuanzia kwenye shule za msingi na sekondari kwenye maeneo yaliyolima kahawa, shule za msingi na sekondari ziwe na mashamba ya kahawa, jambo hili litaongeza uzalishaji; ninaamini ndani ya kipindi kifupi, uzalishaji, utaongezeka na kufikia tani 200,000. Amesisitiza Prof. Jamal
Profesa Jamal ameongeza kuwa Bodi ya Kahawa ipo kwenye maboresho makubwa na kudokeza kuwa kwa sasa imeanda mkakati mwengine wa kuwasaidia Wakulima wadogo wa zao la kahawa nchi kuongeza matumizi ya mbolea, ambapo ameeleza kuwa Mkulima wa Tanzania anatumia kilo 7 za mbolea kwenye hekta moja; matumizi hayo ni ya chini sana ukilinganisha na nchi ya Vietnam na Brazil ambapo Mkulima anatumia zaidi
ya kilo 143 hadi 310 kwa hekta.
Search This Blog
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
Punguza kilo tano kwa siku saba
NI watu wachache wanaopenda kunenepa, wengi wanapenda miili ya wastani kwa kuwa unene si mzuri. Ukiwa mnene si tu kwamba unakaribisha m...
-
Kiwanja kinauzwa kipo Dodoma Mahungu njia ya kwenda Singida kabala hujafika NALA. Kiwanja ni cha Makazi kinaukubwa wa Sqm 450 ( 15 X...
-
Akionekana kwa mara ya kwanza kwa umma tangu aondoke madarakani, aliyekuwa Rais wa Marekani Donald Trump ameweka wazi uwezekano wa kuwania...

No comments:
Post a Comment