Search This Blog

Tuesday, March 10, 2020

Mwanaume mmoja wa London athibitishwa kuwa mtu wa pili duniani kupona HIV


Mwanaume mmoja kutokaLondon Uingereza amethithitishwa kuwa ndiye mtu wa pili kupona virusi vya HIV vinavyosababisha Ukimwi, wamesema madaktari.

Adam Castillejo bado hajapatikana na virusi baada ya kukaa siku 30 bila kumeza dawa za kupunguza makali ya virusi vya HIV zinazofahamika kama anti-retroviral.

Hakupona kutokana na dawa za HIV, hata hivyo, bali kwa tiba ya uboreshaji wa seli alizopewa kwa ajili ya matibabu ya saratani ambayo alikua nayo, limeripoti jarida la kitabibu la the Lancet linaloandika juu ya HIV.

Watoaji wa seli hizo wana geni zisizo za kawaida ambazo zili ziliwapa, na sasa kumpa Bwana Castillejo, ulinzi dhidi ya HIV.

Mwaka 2011,Timothy Brown, "mgonjwa Berlin " alikua ni mtu wa kwanza kuripotiwa kuwa amepona HIV , miaka mitatu na nusu iliyopita baada ya kupata tiba sawa na hiyo.

Tiba ni ipi?
Upandikizaji wa seli zinazoboresha seli nyingine ama Stem-cell transplants unaonekana kuzuia virusi hivyo kuendelea kuwa na uwezo wa kuzaana mwilini ndani ya mwili kwa kuchukua nafasi ya mfumo wenyewe wa seli za kinga za mwili na kutumia seli za mtoaji ambazo zinazuia maambukizi ya HIV.

Adam Castillejo - ambaye sasa ana umri wa miaka 40 "Mgonjwa wa London " ambaye aliamua kutangaza utambulisho wake mwenyewe - hana virusi vya HIV katika damu yake, maji maji ya mwili au nyama za mwili wake, madaktari wake wamesema.

Ni mwaka mmoja sasa baada ya kutangazwa kwa mara ya kwanza kuwa hana virusi vya HIV.

Mtafiti wa Lead Profesa Ravindra Kumar Gupta, kutoka Chuo Kikuu cha Cambridge, ameiambia BBC kuwa : " Hii inaonesha kuwa tiba ya HIV karibia inawezekana''

"Sasa tumekuwa na miaka wawili na nusu ya kutotumia madawa ya kupunguza makali ya HIV.

"Matokeo ya uchunguzi wetu yanaonesha kuwa mafanikio ya matumizi ya upandikizaji wa seli mbadala kutoka kwa mtu mwingine kama tiba ya HIV, kwa mara ya kwanza yaliripotiwa miaka tisa iliyopita katika mgonjwa wa Berlin na yanaweza kunakiliwa."

Tiba hii awali ilitumiwa kutibu saratani ya wagonjwa, sio virusi vya HIV

Na dawa za hivi karibuni za HIV bado zinafanya kazi, ikimaanisha kuwa watu wenye virusi vya HIV wanaweza kuishi maisha marefu na ya afya.

Profesa Gupta anasema: "Ni muhimu kufahamu kuwa tiba hii inayoponya ni ya hatari ya hali ya juu na hutumiwa tu kama tiba ya mwisho kwa wagonjwa wenye HIV ambao wanakabiliwa na hatari ya ukosefu wa damu kutokana na uvimbe wa saratani.

"Kwa hiyo, hii sio tiba ambayo inaweza kutolewa kwa wagonjwa wengi wenye kupata mafanikio ya tiba ya madawa ya kupunguza makali ya HIV -anti-retroviral ."

Lakini inaweza kutoa matumaini ya kupata tiba, katika siku zijazo, kwa upandikizaji wa jeni.

No comments:

Post a Comment

Punguza kilo tano kwa siku saba

  NI watu wachache wanaopenda kunenepa, wengi wanapenda miili ya wastani kwa kuwa  unene si mzuri. Ukiwa mnene si tu kwamba unakaribisha m...