Search This Blog
Wednesday, March 18, 2020
Auawa baada ya kuhisiwa kuwa na virusi vya corona
Polisi huko Kwale wanakisaka kikundi cha watu ambacho kimemuua kijana Hezron Kotin eneo la Kibundani baada ya kumtuhumu kuwa na COVID 19.
Kamanda wa Polisi wa Kaunti ndogo ya Msambweni, Nehemia Bitok alisema kijana huyo alikuwa akitembea kutoka kwa eneo la kunywa na aliingia kwenye kundi la vijana ambao walianza kupiga kelele kuwa ana ugonjwa.
Vijana hao walishambulia mtu huyo wakiwa na silaha na kupelekea kifo chake. Kamanda wa Polisi alisema, waligundua jeraha kubwa kichwani mwake na kumkimbiza katika Hospitali ya Rufaa ya Msambweni.
Polisi wameonya raia dhidi ya kuchukua Sheria mikononi mwao au kutoa madai ya uongo wakati Nchi inachukua hatua za kupambana na janga la COVID 19.
Kaunti ya Kwale imeanza kutoa mafunzo kwa Maafisa wa Afya juu ya kushughulikia kuenea kwa virusi hivyo. Afisa Mkuu wa Afya, Juma Mbete alisema wameweka vituo vitano vya kutengwa katika Kaunti zote tano.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
Punguza kilo tano kwa siku saba
NI watu wachache wanaopenda kunenepa, wengi wanapenda miili ya wastani kwa kuwa unene si mzuri. Ukiwa mnene si tu kwamba unakaribisha m...
-
Kiwanja kinauzwa kipo Dodoma Mahungu njia ya kwenda Singida kabala hujafika NALA. Kiwanja ni cha Makazi kinaukubwa wa Sqm 450 ( 15 X...
-
Akionekana kwa mara ya kwanza kwa umma tangu aondoke madarakani, aliyekuwa Rais wa Marekani Donald Trump ameweka wazi uwezekano wa kuwania...

No comments:
Post a Comment