TUME ya Taifa ya Uchaguzi (NEC), imesema moja ya changamoto zonazoikabili mara kwa mara ni jamii kushindwa kufahamu au kutofautisha kati ya uchaguzi mkuu na wa serikali za mitaa.
Hayo yalielezwa na Makamu Mwenyekiti wa NEC, Jaji Mbarouk M’barouk, wakati akifungua mkutano wa NEC na wadau wa uchaguzi mkoani Lindi.
Jaji Mbarouk alisema yapo maeneo wananchi wake wamekuwa na mtizamo tofauti, wakifikiri uchaguzi wa Serikali za MItaa na uchaguzi zote zinasimamiwa na tume hiyo, jambo ambalo sio la kweli.
Alisema uchaguzi wa Serikali za Mitaa unasimamiwa na Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (Tamisemi), wakati NEC inawajibika na usimamizi wa uchaguzi mkuu pekee, ambao unahusisha Rais, wabunge na madiwani.
“Wananchi walio wengi katika baadhi ya maeneo wanashindwa kutofautisha uchaguzi upi unasimamiwa na Tamisemi na upi Tume ya Taifa ya Uchaguzi,” alisema Jaji Mbarouk.
Alisema kwa kutotambua umuhimu wa jambo hilo, tume imeamua kushirikisha wadau kushiriki katika michakato ya uchaguzi kwa lengo la kuwa karibu nao, ili kujenga imani kwa wananchi na kuweka uwazi wa utekelezaji wa majukumu yake.
Alisema tume inaamini kila kundi la wadau, wakiwamo viongozi wa kisiasa, dini, mila, watu wenye walemavu na wanahabari wana umuhimu wake katika zoezi zima la uchaguzi.
Jaji M’barouk alisema uboreshaji wa daftari la kudumu la wapigakura unasimamiwa na kuendeshwa kwa mujibu wa sheria, kanuni na maelekezo ya tume, huku akisisitiza viongozi wa vyama vya siasa watapatiwa maelekezo kwa mfumo wa vijitabu.
Pia aliviomba vyama vya siasa na wadau wengine kuzingatia sheria za uchaguzi, kanuni za uboreshaji daftari na maelekezo kwa vyama vya siasa, huku akiwataka kutoa taarifa sahihi na kwa wakati ili kila mwananchi mwenye sifa ya kuandikishwa ajiandikishe.
Uboreshaji wa Daftari la Kudumu la Wapigakura unafanyika kwa kutumia teknolojia ya kielektroniki ya Biometriki (BRV) ambavyo huchukuwa taarifa za kibaiolojia na kuzihifadhi katika kanzi data (Database).
Uboreshaji huo kwa mkoa wa Lindi kwa mujibu wa NEC unatarajia kufanyika kwa siku saba, kuanzia Januari 12 hadi 18, mwaka huu.
Search This Blog
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
Punguza kilo tano kwa siku saba
NI watu wachache wanaopenda kunenepa, wengi wanapenda miili ya wastani kwa kuwa unene si mzuri. Ukiwa mnene si tu kwamba unakaribisha m...
-
Kiwanja kinauzwa kipo Dodoma Mahungu njia ya kwenda Singida kabala hujafika NALA. Kiwanja ni cha Makazi kinaukubwa wa Sqm 450 ( 15 X...
-
Akionekana kwa mara ya kwanza kwa umma tangu aondoke madarakani, aliyekuwa Rais wa Marekani Donald Trump ameweka wazi uwezekano wa kuwania...

No comments:
Post a Comment