Na Amiri kilagalila-Njombe
Waziri wa kilimo nchini Japhet Hasunga ameziagiza taasisi ya kudhibiti ubora wa Mbegu (TOSC) na taasisi ya utafiti wa viuatilifu vya kudhibiti visumbufu katika ukanda wa Kitropiki (TPRI),kuhakikisha wanazunguka kwenye mabohari na mawakala nchi nzima kuona usahihi wa madawa na mbegu zinazotumika.
Waziri hasunga ametoa agizo hilo mkoani Njombe wakati akikagua uwepo wa pembejeo kwa wauzaji wa pembejeo mjini Makambako.
“Laikini taasisi ya TPRI pamoja TOSC nitumie fursa hii kuwaagiza wazunguke katika maeneo mbalimbali kwenye bohari kwa mawakala nchi nzima,wakague waone usahihi wa mbegu lakini waone usahihi wa madawa yanayotumika yote,na wale ambao itaonekana wamevunja taratibu na sheria za nchi yaani wameleta vitu feki basi hatua kali zichukuliwe kwa mujibu wa sheria na waadhibiwe kwa kadri itakavyowezekana”alisema Japhet Hasunga
Katika hatua nyingine amemuagiza TBA kumsimamia mkandarasi wa ujenzi wa maghala ya kuhifadhia mahindi yanayojengwa mjini Makambako kuhakikisha mradi huo hadi kufikia 30-6-2020 uwe umekamilika na kuanza kutumika.
“Kufikia tarehe 30 June mhakikishe wanakamilisha wakabidhi ili Julai tuanze kutumia hivi vihenge hatutakuwa na sababu zingine zozote za kuongeza muda,na kwasababu huu mradi ulitakiwa uwe umekamilika disemba kumekuwa na changamoto za hapa na pale sasa tumepeleka June,nah ii itatusaidia sasa tuanze kupambana na sumu kuvu”alisema Japhet Hasunga
Search This Blog
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
Punguza kilo tano kwa siku saba
NI watu wachache wanaopenda kunenepa, wengi wanapenda miili ya wastani kwa kuwa unene si mzuri. Ukiwa mnene si tu kwamba unakaribisha m...
-
Kiwanja kinauzwa kipo Dodoma Mahungu njia ya kwenda Singida kabala hujafika NALA. Kiwanja ni cha Makazi kinaukubwa wa Sqm 450 ( 15 X...
-
Akionekana kwa mara ya kwanza kwa umma tangu aondoke madarakani, aliyekuwa Rais wa Marekani Donald Trump ameweka wazi uwezekano wa kuwania...

No comments:
Post a Comment