Search This Blog

Saturday, January 4, 2020

Rais Trump adai Marekani itavilenga vituo 52 vya Iran

Rais Donald Trump wa Marekani ameonya kuwa nchi yake itayashambulia haraka na vikali maeneo 52 ya Iran iwapo Jamhuri hiyo ya Kiislam itafanya mashambulizi dhidi ya raia wa Marekani na mali zake kulipiza kisasi kwa mauaji ya Jenerali Qassem Soleimani.

Katika ujumbe wa kitisho kupitia ukurasa wa Twitter, Trump amesema maeneo yatakayolengwa ni yale yaliyo muhimu kwa Iran na utamaduni wake na kuonya Marekani haiko tayari kuendelea kutishwa na Iran.

Ujumbe huo wa Trump unafutia onyo la makundi ya wanamgambo yanayoiunga mkono Iran la kuvishambulia vituo vya Marakani nchini Iraq kutokana na mauaji ya kamanda huyo muhimu wa jeshi la Iran.

Katika ishara za mwanzo za uwezekano wa kulipa kisasi, makombora mawili yalilipiga eneo lililo karibu na ubalozi wa Marekani mjini Baghdad siku ya Jumamosi.

Makombora mengine mawili yaliishambulia kambi ya kijeshi ambayo inahifadhi wanajehsi wa Marekani lakini hakuna athari kubwa zilizoripotiwa.

No comments:

Post a Comment

Punguza kilo tano kwa siku saba

  NI watu wachache wanaopenda kunenepa, wengi wanapenda miili ya wastani kwa kuwa  unene si mzuri. Ukiwa mnene si tu kwamba unakaribisha m...