Malkia Elizabeth wa Uingereza jana ameelezea kuhuzunishwa na janga la moto linaloikumba Australia na kutuma salamu zake pole kwa raia wa nchi hiyo na wale wanaopambana kukabiliana na moto unaoendelea kuwaka.
Malkia Elizabeth anayetawala pia Australia ametuma salamu hizo wakati moto usiodhibitika ukiendelea kulimbuka eneo la pwani ya mashariki ya nchi hiyo ukiharibu nyumba na kusababisha kifo cha mtu mmoja.
Maelfu ya watu wamelazimka kuyahama makaazi yao huku idara ya hali ya hewa ya Australia ikisema hali inazidi kuwa mbaya baada ya mabadiliko ya upepo kusambaza moto zaidi.
Serikali ya Australia imetangaza kupeleka askari wa akiba kusaidia vikosi vya zima moto pamoja kuongeza meli ya tatu ya kijeshi yenye uwezo wa kutoa msaada wa kiutu.
Search This Blog
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
Punguza kilo tano kwa siku saba
NI watu wachache wanaopenda kunenepa, wengi wanapenda miili ya wastani kwa kuwa unene si mzuri. Ukiwa mnene si tu kwamba unakaribisha m...
-
Kiwanja kinauzwa kipo Dodoma Mahungu njia ya kwenda Singida kabala hujafika NALA. Kiwanja ni cha Makazi kinaukubwa wa Sqm 450 ( 15 X...
-
Akionekana kwa mara ya kwanza kwa umma tangu aondoke madarakani, aliyekuwa Rais wa Marekani Donald Trump ameweka wazi uwezekano wa kuwania...

No comments:
Post a Comment