Search This Blog

Saturday, December 28, 2019

Waziri wa Kilimo aagiza kukamatwa kwa mtu huyu na kufunguliwa mashtaka ya uhujumu uchumi


Waziri wa Kilimo Mhe Japhet Hasunga (Mb) ameliagiza jeshi la Polisi nchini kumkamata na kumfungulia mashtaka ya uhujumu uchumi Kaimu Mrajisi wa vyama vya ushirika mkoa wa Rukwa Anosisye Mbetwa.

Waziri Hasunga ametoa agizo wakati akizungumza kwenye kikao cha kazi kilichowakutanisha viongozi na wanachama wa vyama vya ushirika (AMCOS) katika ukumbi wa mikutano kwenye ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Rukwa.

Mrajisi huyo ameweka kizuizini kwa kubainika kushiriki kuingia mkataba na Kampuni ya kusambaza mbolea ya ELI AGROVENT CO kinyume na taratibu za serikali hali iliyopelekea chama kikuu cha ushirika mkoani humo Ufipa Cooperative Union (UCU) kutapeliwa shilingi Milioni 277 huku wanachama wake wakiendelea kuhangaika juu ya upatikanaji wa mbolea.

Pia Mhe Hasunga ameagiza kukamatwa na kufunguliwa kesi ya uhujumu Uchumi Mkurugenzi Mtendaji wa kampuni ya kusambaza mbolea ya ELI AGROVENT CO Bw Elias Ndomba kutokana na kuwauzia wakulima mbolea kinyume na bei elekezi ya serikali iliyotangazwa hivi karibuni.

No comments:

Post a Comment

Punguza kilo tano kwa siku saba

  NI watu wachache wanaopenda kunenepa, wengi wanapenda miili ya wastani kwa kuwa  unene si mzuri. Ukiwa mnene si tu kwamba unakaribisha m...