Search This Blog

Saturday, December 28, 2019

Gigy Money Sibadili Hadi Kaburini



MREMBO anayefanya poa kunako anga la Bongo Fleva, Gift Stanford ‘Gigy Money’ amesema wanaomsema waendelee kumsema kwa kuwa hawezi kubadilika mpaka anaingia kaburini.



Akizungumza na Risasi Jumamosi, Gigy amesema watu wengi wamekuwa wakimsema na kumtaka abadilike kwani ana matukio ya ajabuajabu kila uchwao wakati yeye anaona bila vimbwanga hakuna ambaye angemfahamu. “Utamsikia mtu badilika sasa najibadilishaje si ndiyo kuishi maisha feki hayo?

 

Hata mtoto wangu akikua anatakiwa ajue mama alikuwa mtu wa aina gani,” alisema Gigy ambaye miezi michache iliyopita alisema amebadilika na kuanza kwenda kanisani.

Stori: Imelda Mtema





No comments:

Post a Comment

Punguza kilo tano kwa siku saba

  NI watu wachache wanaopenda kunenepa, wengi wanapenda miili ya wastani kwa kuwa  unene si mzuri. Ukiwa mnene si tu kwamba unakaribisha m...