Search This Blog
Thursday, December 26, 2019
Waziri Mkuu wa Sudan kuwafikisha Mahakamani wahalifu wa mauaji ya kimbari
Waziri Mkuu wa Sudan Bw. Abdalla Hamdok aahidi kuwafikisha mahakamani wanaohusika na mauaji ya kimbari.
Bw. Hamdok amesema hayo akitoa hotuba katika mkutano wa kuadhimisha mwaka mmoja wa maandamano ya Desemba ya Sudan, huku akisema haki itatendeka, sheria itafuata mkondo dhidi ya wauaji wote.
Ameongeza kuwa uhalifu wa kivita na mauaji ya kimbari hauna ukomo wa muda wa kisheria, juhudi zitafanyika kuhakisha wahalifu wote wanafikishwa mahakamani na heshima kwa familia za wafiwa inarejeshwa.
Watu wa Sudan wanasherehekea maadhimisho ya mwaka mmoja tangu maandamano yafanyike Desemba 19 mwaka jana. Kutokana na shinikizo mitaani, jeshi la Sudan Aprili 11 lilimwondoa madarakani rais wa zamani Omar al-Bashir na kuunda baraza la kijeshi kusimamia mambo ya nchi.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
Punguza kilo tano kwa siku saba
NI watu wachache wanaopenda kunenepa, wengi wanapenda miili ya wastani kwa kuwa unene si mzuri. Ukiwa mnene si tu kwamba unakaribisha m...
-
Kiwanja kinauzwa kipo Dodoma Mahungu njia ya kwenda Singida kabala hujafika NALA. Kiwanja ni cha Makazi kinaukubwa wa Sqm 450 ( 15 X...
-
Akionekana kwa mara ya kwanza kwa umma tangu aondoke madarakani, aliyekuwa Rais wa Marekani Donald Trump ameweka wazi uwezekano wa kuwania...

No comments:
Post a Comment