Search This Blog
Thursday, December 26, 2019
Simiyu Warriors yatambulisha kikosi chake kuelekea Taifa Cup
Mashindano ya mpira wa kikapu ngazi ya taifa, Taifa Cup yanatarajia kuanza kutimua vumbi Desemba 27 Mkoani Simiyu ambapo timu kumi kutoka mikoa ya Tanzania bara na Zanzibar zinatarajia kushiriki.
Kuelekea michuano hiyo, timu mwenyeji leo imefanya utambulisho rasmi wa kikosa chao kwa wakazi wa mkoa huo kwa kucheza mchezo wa kirafiki katika moja ya barabara za katikati ya mji wa Bariadi yalipo makao makuu ya mkoa huo.
Zena Mchujuko mratibu wa mchezo wa mpira wa kikapu mkoani Simiyu amesema tayari viongozi wa chama cha mpira wa kikapu taifa wamekwishawasili na timu tatu kati ya kumi zimekwishafika tayari kwa ajili ya mashindano hayo.
Kidson Ndunguru kocha wa timu ya mkoa wa Simiyu amesema kufuatia ujio wa mashindano hayo timu ya Simiyu warriors imeamua kutambulisha wachezaji wake kwa kuonesha namna mchezo unavyochezwa katikati ya mji ili kuhamasisha wananchi kujitokeza kwa wingi uwanja wa halmashauri ya mji wa Bariadi yatakapofanyika mashindano hayo kwa muda wa siku tano.
Timu ya Simiyu haikufanya vizuri katika mashindano haya mwaka jana, Humphrey Rwekaza nahodha wa timu ya Simiyu Warriors amesema mwaka huu wamefanya maandalizi ya kutosha ili kuuwakilisha mkoa vyema.
Mashabiki wa mpira wa Kikapu mkoani humo wanasema bado wana imani na timu yao.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
Punguza kilo tano kwa siku saba
NI watu wachache wanaopenda kunenepa, wengi wanapenda miili ya wastani kwa kuwa unene si mzuri. Ukiwa mnene si tu kwamba unakaribisha m...
-
Kiwanja kinauzwa kipo Dodoma Mahungu njia ya kwenda Singida kabala hujafika NALA. Kiwanja ni cha Makazi kinaukubwa wa Sqm 450 ( 15 X...
-
Akionekana kwa mara ya kwanza kwa umma tangu aondoke madarakani, aliyekuwa Rais wa Marekani Donald Trump ameweka wazi uwezekano wa kuwania...


No comments:
Post a Comment