Search This Blog

Thursday, December 26, 2019

Liverpool yazidi kutoa kichapo Ligi Kuu England


Liverpool imeendeleza Ubabe Ligi Kuu England baada ya Kuitandika timu inayoifuatia kwa karibu kwenye msimamo Leicester City ikiwa nafasi ya pili Mabao 4 kwa bila katika dimba la King Power

Magoli ya Liverpool yamefungwa na Roberto Firmino dakika 31, bao la pili likifungwa na Milner kwa mkwaju wa Penalt huku Firmino akirudi tena wavuni kufunga bao la tatu na bao la nne likifungwa na Alexander Anord ndani ya dakika 78 akipokea pasi safi kutoka kwa Sadio Mane

Liverpool inaendelea kushika usukani wa msimamo wa Ligi kwa kuwa na alama 52 huku Leicester ikibaki na alama 39, Manchester city yenye alama 38 itashuka dimbani dhidi ya Wolverhampton, ikishinda mchezo huo itasogea hadi nafasi ya pili.



No comments:

Post a Comment

Punguza kilo tano kwa siku saba

  NI watu wachache wanaopenda kunenepa, wengi wanapenda miili ya wastani kwa kuwa  unene si mzuri. Ukiwa mnene si tu kwamba unakaribisha m...