Search This Blog
Thursday, December 5, 2019
Watoto 56 wafanyiwa upasuaji wa Moyo kambi maalum JKCI
Madaktari bingwa wa magonjwa ya moyo kwa watoto wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) na wenzao kutoka King Salman Humanitarian Aid and Relief Center wa nchini Saud Arabia wakimfanyia upasuaji wa bila kufungua kifua na kuziba tundu la moyo wa mtoto kwa kutumia mtambo wa Cathlab wakati wa kambi maalum ya matibabu inayofanyika katika Taasisi hiyo.
Jumla ya watoto 33 wamefanyiwa upasuaji mdogo wa bila kufungua kifua ambapo hali zao zinaendelea vizuri na wengine wameruhusiwa kurudi nyumbani.
Madaktari bingwa wa magonjwa ya moyo kwa watoto wa JKCI kwa kushirikiana na wenzao kutoka King Salman Humanitarian Aid and Relief Center wa nchini Saud Arabia wakimfanyia mtoto upasuaji mkubwa wa kusimamisha moyo na kurekebisha mishipa ya damu ya moyo katika kambi maalum ya matibabu inayoendelea katika Taasisi hiyo.
Jumla ya watoto 23 wenye matatizo ya moyo wamefanyiwa upasuaji mkubwa na hali zao zinaendelea vizuri.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
Punguza kilo tano kwa siku saba
NI watu wachache wanaopenda kunenepa, wengi wanapenda miili ya wastani kwa kuwa unene si mzuri. Ukiwa mnene si tu kwamba unakaribisha m...
-
Kiwanja kinauzwa kipo Dodoma Mahungu njia ya kwenda Singida kabala hujafika NALA. Kiwanja ni cha Makazi kinaukubwa wa Sqm 450 ( 15 X...
-
Akionekana kwa mara ya kwanza kwa umma tangu aondoke madarakani, aliyekuwa Rais wa Marekani Donald Trump ameweka wazi uwezekano wa kuwania...


No comments:
Post a Comment