Search This Blog

Thursday, December 5, 2019

Binti aliyebakwa kisha kuchomwa moto adaiwa kupigania uhai wake


Binti mwathirika wa ubakaji mwenye umri wa miaka 23 aliyedaiwa kubakwa na wanaume wawili kwa sasa anapigania maisha yake baada ya kuchomwa moto akiwa njiani kuelekea mahakamani kusikiliza kesi yake huko kaskazini mwa India.

Mwanamke huyo alikutwa na janga hilo akiwa njiani kwenda kusikiliza kesi hiyo aliyoifungua dhidi ya wanaume wawili waliombaka mwezi Machi huko in Uttar Pradesh.

Kwa sasa mwanamke huyo yuko taabani hospitalini ambako anapatiwa matibabu ya majereha yake ya moto. Jumla ya wanaume watano wamekamatwa wakiwemo wawili waliotuhumiwa na mwathirika huyo kwa tuhuma za kumchoma moto mwanamke huyo, polisi wamethibitisha.

Tukio hilo lilimkuta mwanamke huyo akiwa njiani kwenda kituo cha treni wakati kundi la wanaume lilipojitokeza na kumshambulia na kisha kumbana kwenye eneo jirani na kituo hicho kisha kumchoma moto kwa mujibu wa vyombo vya habari vya ndani.

Madaktari wanaomtibu katika Hospitali ya mjini Lucknow wamesema mwanamke huyo ameungua kwa asilimia 90 na alikuwa akitarajiwa kusafirishwa kwa njia ya anga kupelekwa mji mkuu wa nchi hiyo Delhi, kwaajili ya matibabu zaidi.

Tukio hilo limetokea wilayani Unnao ambayo hivi karibuni imekuwa ikikabiliwa na kesi za ubakaji.Hivi karibuni pia polisi walifungua jalada la uchunguzi dhidi ya mbunge wa Chama Tawala ambaye mwezi Julai alidaiwa kumbaka mwanamke mmoja ambaye baadaye mwanamke huyo alijeruhiwa vibaya katika ajali ya gari huku mama zake wadogo wawili wakiuawa na wakili wake akijeruhiwa pia.

Hata hivyo tukio hilo la hivi karibuni limeamsha vurugu na maandamani nchini humo wakizitaka mamlaka husika kuchukua hatua.

No comments:

Post a Comment

Punguza kilo tano kwa siku saba

  NI watu wachache wanaopenda kunenepa, wengi wanapenda miili ya wastani kwa kuwa  unene si mzuri. Ukiwa mnene si tu kwamba unakaribisha m...