Search This Blog

Thursday, December 5, 2019

TANZIA: Mchezaji wa zamani Yanga, Ally Yussuf 'Tigana' afariki dunia


Kiungo wa zamani wa kimataifa wa Tanzania, Ally Yussuf Suleiman ‘Tigana’ amefariki dunia hapo jana katika hospitali ya Amana mjini Dar es Salaam baada ya kuugua kwa muda mfupi.

Kwa mujibu wa rafiki wa karibu wa marehemu, Mwanamtwa Kihweli msiba upo nyumbani kwake Kimara na taarifa zaidi zitatolewa baada ya kikao cha wanandugu.

Timu yake ya kwanza ni Shaurimoyo Kids kabla ya kujiunga na Manyema Rangers mwaka 1989 ambako alicheza hadi mwaka 1991 alipochukuliwa na Pan Africans ikiwa Daraja la Pili (sasa Daraja la Kwanza) wakaipandisha Ligi Kuu mwaka 1993.

Mwaka 1994 akachukuliwa na Yanga SC ambako alicheza kwa msimu mmoja kabla ya kuhamia Simba SC alikocheza hadi mwaka 1997 akaenda Cadets ya Maurtius alikocheza hadi mwaka 2000 aliporejea Simba SC. 

Alicheza kwa msimu mmoja Simba SC kabla ya kurejea Yanga SC ambako alicheza hadi mwaka 2004 alipokwenda kumalizia soka yake Twiga SC ya Kinondoni. Jina la Tigana alipewa kutokana na kufananishwa na kiungo wa kimataifa wa Ufaransa miaka ya 1980, Jean Pierre Tigana.
Mungu ampumzishe kwa amani marehemu Ally Yussuf Suleiman ‘Tigana’.

No comments:

Post a Comment

Punguza kilo tano kwa siku saba

  NI watu wachache wanaopenda kunenepa, wengi wanapenda miili ya wastani kwa kuwa  unene si mzuri. Ukiwa mnene si tu kwamba unakaribisha m...