Search This Blog
Thursday, December 5, 2019
BMT wapiga marufuku Marathon bila kibali
Baraza la Michezo la Taifa (BMT) limepiga marufuku mbio za marathoni na mbio nyingine za barabarani zinazofanyika bila kibali kutoka katika baraza hilo kuanzia Januari Mosi 2020.
Kaimu Katibu Mtendaji wa baraza hilo Neema Msitha amesema vibali hivyo vitatolewa baada ya baraza kujiridhisha kuwa muandaaji wa mbio hizo amekidhi matakwa ya uendeshaji wa mbio hizo.
Katika hatua nyingine Mashindano ya riadha kwa wanawake “Ladies First 2019” yanatarajia kufanyika Disemba 7 hadi 8, 2019 kwenye uwanja wa Taifa jijini Dar es salaam.
Wanariadha wa kike na viongozi zaidi ya 200 kutoka mikoa yote ya Tanzania Bara na visiwani watashiriki huku Sudani Kusini wakishiriki kama waalikwa.
Mashindano hayo ambayo yameandaliwa na BMT kwa kushirikiana na Taasisi ya Ushirikiano wa Kimataifa ya Japani (JICA) pamoja na Shirikisho la Riadha Tanzania yatashuhudiwa pia na wanafunzi 1,000 kutoka baadhi ya shule za msingi na sekondari kutoka Manispaa ya Temeke.
Baraza limeomba wananchi wote wa Wilaya ya Temeke na maeneo yote ya Jiji la Dar es Salaam kujitokeza kwa wingi siku ya mashindano kuwashangilia na kuwapa hamasa wanariadha hao, kwani hakutakuwa na kiingilio chochote.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
Punguza kilo tano kwa siku saba
NI watu wachache wanaopenda kunenepa, wengi wanapenda miili ya wastani kwa kuwa unene si mzuri. Ukiwa mnene si tu kwamba unakaribisha m...
-
Kiwanja kinauzwa kipo Dodoma Mahungu njia ya kwenda Singida kabala hujafika NALA. Kiwanja ni cha Makazi kinaukubwa wa Sqm 450 ( 15 X...
-
Akionekana kwa mara ya kwanza kwa umma tangu aondoke madarakani, aliyekuwa Rais wa Marekani Donald Trump ameweka wazi uwezekano wa kuwania...

No comments:
Post a Comment