Search This Blog

Sunday, December 8, 2019

Washikiliwa na Polisi wakituhumiwa kushiriki mauaji kisa ushirikina


Polisi Mkoani Mbeya wanawashikilia Watu watatu kwa tuhuma za mauaji ya John Mwakarundwa(62) Mkazi wa Kijiji cha Nkunga, Rungwe tukio ambalo linahusishwa na imani za kishirikina.

Kamanda wa Polisi Mbeya Ulrich Matei amesema Watuhumiwa walimvamia Mwakarundwa na kumkatakata na vitu vyenye ncha kali maeneo ya kisogoni, taya la kushoto na tumboni hadi kufariki.

RPC Matei amesema historia inaonesha Mwakarunda alikuwa anatuhumiwa kwenda kununua uchawi Malawi hivyo Wananchi wa eneo hilo walikuwa na hasira nae wakidai anawatesa Kijijini hapo.

"Watuhumiwa wanadai wamefanya hivyo ili kulipiza kisasi na baada ya kuuawa kwake Wananchi walikuwa wanashangilia wakifurahia kifo chake, Serikali haiwezi kujiingiza kwenye mambo hayo tutawahoji na kuwafikisha Mahakamani" amesema.

No comments:

Post a Comment

Punguza kilo tano kwa siku saba

  NI watu wachache wanaopenda kunenepa, wengi wanapenda miili ya wastani kwa kuwa  unene si mzuri. Ukiwa mnene si tu kwamba unakaribisha m...