Search This Blog
Sunday, December 8, 2019
Shule aliyosoma Mwl. Nyerere kukarabatiwa na serikali
Serikali imeamua kuifanyia ukarabati mkubwa Shule ya Msingi Mwisenge, ambayo alisoma Baba wa Taifa, Mwl. Julius Kambarage Nyerere ili iwe sehemu ya historia ya Tanzania.
Akizungumza mara baada ya kutembelea shule hiyo, Waziri Mkuu Kassim Majaliwa, amesema Shule hiyo ambayo ipo Manispaa ya Musoma wanaikarabati ili iwe sehemu ya historia ya Mwalimu Nyerere, pamoja na historia ya Tanzania kwa ujumla.
“Shule hiyo haiwezi kubeba historia ya Mwalimu Nyerere, endapo majengo na miundombinu ya shule hiyo haitakarabatiwa na kujengwa upya, Mipango ya kuifanya shule hiyo iwe sehemu ya historia ya Tanzania inaendelea serikalini na kwamba historia ya Baba wa Taifa itapatikana shuleni hapo.” amesema Waziri Mkuu.
Waziri Mkuu amesema kuwa uamuzi wa kuifanya shule hiyo iwe yenye historia hapa nchini, inatokana na uwepo wa viongozi mbalimbali waliosomea hapo akiwemo Waziri Mkuu Mstaafu wa Tanzania, Jaji Joseph Warioba pamoja na Mzee Joseph Butiku.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
Punguza kilo tano kwa siku saba
NI watu wachache wanaopenda kunenepa, wengi wanapenda miili ya wastani kwa kuwa unene si mzuri. Ukiwa mnene si tu kwamba unakaribisha m...
-
Kiwanja kinauzwa kipo Dodoma Mahungu njia ya kwenda Singida kabala hujafika NALA. Kiwanja ni cha Makazi kinaukubwa wa Sqm 450 ( 15 X...
-
Akionekana kwa mara ya kwanza kwa umma tangu aondoke madarakani, aliyekuwa Rais wa Marekani Donald Trump ameweka wazi uwezekano wa kuwania...

No comments:
Post a Comment