Search This Blog

Tuesday, December 10, 2019

Tafiti zinazofanyika nchini zatakiwa kujibu changamoto za Watanzania


Naibu Waziri Elimu, Sayansi na Teknolojia Mhe. William Ole Nasha amesema tafiti zinazofanyika nchini zinatakiwa kujibu changamoto zinazoikabili jamii ya watanzania na Afrika kwa ujumla.

Naibu Waziri Ole Nasha ameyasema hayo Jijini Arusha akifungua Mkutano wa kumi wa Kimataifa wa Jumuiya ya Watafiti katika Malighafi Afrika (AMRS- 2019) kwa niaba ya Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe Samia Suluhu Hassan.

Kiongozi huyo amesema Tanzania imejikita katika ujenzi wa uchumi wa kati kupitia viwanda hivyo ni lazima tafiti zinazofanyika zijikite kwenye maeneo ya sayansi, teknolojia na ubunifu ili zitumike kuimarisha utengenezaji bidhaa na huduma zinazoendana na azma hiyo.

“Ni nani anaamua nini kifanyiwe tafiti, je tafiti hizo ni za kuwafaidisha waliopo nje ya nchi au watanzania? ni lazima tujikite kwenye tafiti zitakazosaidia kutatua changamoto zilizopo katika mataifa yetu na hivyo sisi wenyewe tuwe waanzilishi wa ajenda ya utafiti kulingana na mahitaji,” alisema Naibu Wazirii Ole Nasha

Kwa upande wake Rais wa Jumuiya ya Watafiti katika Malighafi ambae pia ni Mhadhiri wa Chuo Kikuu cha Sayansi na Teknolojia cha Nelson Mandela, Prof. Hulda Swai amesema mkutano huo pamoja na mambo mengine utaainisha na kujadili maeneo ya vipaumbele vya tafiti ambavyo vitatumiwa na Vyuo Vikuu pamoja na Taasisi za kitafiti.




No comments:

Post a Comment

Punguza kilo tano kwa siku saba

  NI watu wachache wanaopenda kunenepa, wengi wanapenda miili ya wastani kwa kuwa  unene si mzuri. Ukiwa mnene si tu kwamba unakaribisha m...