Search This Blog

Tuesday, December 10, 2019

Ambaka mtoto wa darasa la sita hadi kumuua, ajisalimisha Polisi


Mponjoli Lisa, anashikiliwa na Jeshi la Polisi kwa madai ya kumbaka binti wa darasa la sita Shule ya Msingi Pugu Kajiungeni hadi kumuua.

Akizungumza Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kipolisi Ilala, Zuberi Chembela amethibitisha kutokea kwa tukio hilo na kwamba watu wanne wanashikiliwa na polisi.

Mwenyekiti wa mtaa wa Pugu Bombani, Amanzi Bungara amesema tukio hilo limetokea Jumapili Desemba 8, 2019 na kudai kuwa Lisa baada ya kufanya tukio hilo alijisalimisha kituo cha polisi Stakishari na kukiri kufanya kitendo hicho.

“Lisa alikwenda nyumbani kwa huyo binti na kuomba amsindikize dukani na walipokuwa njiani alimfanyia kumfanyia unyama huo. Tumemzika leo jioni katika makaburi ya Mwakanga.”

“Kutokana na tukio hili limewaagiza wakazi wa mtaa wangu kuorodhesha majina ya wapangaji wao ili niwajue, lakini tumepanga kuanzisha ulinzi shirikishi,” amesema Bungara.




No comments:

Post a Comment

Punguza kilo tano kwa siku saba

  NI watu wachache wanaopenda kunenepa, wengi wanapenda miili ya wastani kwa kuwa  unene si mzuri. Ukiwa mnene si tu kwamba unakaribisha m...