Rais wa Marekani Donald Trump amesema jana kuwa nchi yake itatiliana saini na China kile kinachojulikana kama awamu ya kwanza ya makubaliano ya kibiashara baada ya mazungumzo kati ya mataifa hayo kukamilika.
Awamu ya kwanza ya makubaliano ya kibiashara ilitangazwa mapema mwezi Disemba kama sehemu ya juhudi za kumaliza miezi kadhaa ya vita vya kibishara kati ya mataifa hayo mawili yenye chumi kubwa iliyoteteresha masoko na ukuaji wa uchumi duniani.
Kulingana na waziri wa fedha wa Marekani Steven Mnuchin makubaliano hayo yanaweza kutiwa saini mapema mwezi Januari na kwamba sasa yanafanyiwa marekebisho ya mwisho.
Chini ya makubaliano hayo Marekani itaridhia kupunguza baadhi ya ushuru kwa ahadi kuwa China itaongeza ununuaji wa bidhaa za kilimo kutoka Marekani.
Search This Blog
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
Punguza kilo tano kwa siku saba
NI watu wachache wanaopenda kunenepa, wengi wanapenda miili ya wastani kwa kuwa unene si mzuri. Ukiwa mnene si tu kwamba unakaribisha m...
-
Kiwanja kinauzwa kipo Dodoma Mahungu njia ya kwenda Singida kabala hujafika NALA. Kiwanja ni cha Makazi kinaukubwa wa Sqm 450 ( 15 X...
-
Akionekana kwa mara ya kwanza kwa umma tangu aondoke madarakani, aliyekuwa Rais wa Marekani Donald Trump ameweka wazi uwezekano wa kuwania...

No comments:
Post a Comment