Bunge la Cuba jana limemteua Manuel Marrero kuwa waziri mkuu wa kisiwa hicho chini ya katiba mpya inayolenga kugawanya madaraka kupitia wadhifa huo uliowahi kushikiliwa na Fidel Castro.
Marrero, waziri wa zamani wa utalii, atakuwa waziri mkuu wa kwanza wa Cuba tangu mwaka 1976 na atagawana madaraka ya uongozi na rais Miguel Diaz-Canel. Mtaalamu huyo wa usanifu majengo mwenye umri wa miaka 56 alijipatia umashuhuri ndani ya shirika la utalii linaloongozwa na jeshi kabla ya kuwa waziri wa Utalii wa Cuba mwaka 2004.
Fidel Castro, kiongozi wa zamani wa Cuba alikuwa waziri mkuu hadi 1976 wakati cheo hicho kilipofutwa na yeye kuchaguliwa kuwa rais na mwenyekiti wa chama cha kikomunisti nchini humo.
Search This Blog
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
Punguza kilo tano kwa siku saba
NI watu wachache wanaopenda kunenepa, wengi wanapenda miili ya wastani kwa kuwa unene si mzuri. Ukiwa mnene si tu kwamba unakaribisha m...
-
Kiwanja kinauzwa kipo Dodoma Mahungu njia ya kwenda Singida kabala hujafika NALA. Kiwanja ni cha Makazi kinaukubwa wa Sqm 450 ( 15 X...
-
Akionekana kwa mara ya kwanza kwa umma tangu aondoke madarakani, aliyekuwa Rais wa Marekani Donald Trump ameweka wazi uwezekano wa kuwania...

No comments:
Post a Comment