Search This Blog

Saturday, December 21, 2019

Rais Macron aahidi mapambano zaidi dhidi ya makundi ya itikadi kali

Rais wa Ufaransa Emanuel Macron jana ameahidi kuongeza mapambano dhidi ya makundi ya itikadi kali magharibi ya Afrika wakati vikosi vya nchi yake vikitangaza kuwauwa wanamgambo 33 wa itakadi kali nchini Mali.

Akizungumza kwenye mkutano na waandishi habari mjini Abidjan, nchini Ivory Coast, Macron amesema ni lazima kuendelea kuungana na kutia nia ya kukabili kitisho cha Itikadi kali kwenye kanda hiyo.

Jumamosi ilikuwa siku ya pili ya ziara ya siku tatu ya Macron kwenye mataifa ya Ivory Coast na Niger ambayo imetawaliwa na kuongezeka kitisho cha makundi ya itakadi kali katika eneo la Afrika Magharibi.

Katika hatua nyingine, rais wa Ivory Coast Allassane Outtara aliyekuwa mwenyeji wa Macron mjini Abdijan, ametanganza mageuzi makubwa ya sarafu ya CFA inayotumiwa na mataifa nane ya magharibi na kati ya Afrika.

Mageuzi hayo yanajumuisha kuondolewa maafisa wote wa Ufaransa kutoka vyombo vinavyosimamia sarafu hiyo pamoja na sharti la kuwekwa nusu ya akiba ya fedha za kigeni za nchi wanachama nchini Ufaransa.

No comments:

Post a Comment

Punguza kilo tano kwa siku saba

  NI watu wachache wanaopenda kunenepa, wengi wanapenda miili ya wastani kwa kuwa  unene si mzuri. Ukiwa mnene si tu kwamba unakaribisha m...