Search This Blog

Saturday, December 21, 2019

Kampuni inayoshiriki ujenzi wa Nord 2 yasitisha shughuli zake kutokana na vikwazo vya Marekani

Kampuni inayoendesha meli za ujenzi wa bomba jipya la gesi kutoka Urusi kwenda Ujerumani imetangaza jana kusitisha shughuli zake baada ya rais wa Marekani kutia saini sheria inayotishia vikwazo dhidi ya kampuni zinazoshiriki ujenzi wa mradi huo.

Kampuni hiyo ya Allseas imesema inasitisha kazi zote za kusambaza mabomba katika mradi wa Nord 2 wakati ikitafuta ufafanuzi kutoka mamlaka za Marekani kuhusu matakwa ya sheria mpya.

Siku ya Ijumaa rais Donald Trump alitia saini sheria itakayoweka vikwazo kwa watu na kampuni za meli zinazoshiriki ujenzi bomba la gesi la Nord 2 katika bahari ya Baltiki.

Marekani pamoja na mataifa Ulaya Masharriaki, ni wakosoaji wakubwa wa ujenzi wa bomba hilo ambalo Washington inasema litaongeza utegemezi wa bara Ulaya kwenye nishati ya Urusi.

Ujenzi wa bomba la Nord 2 tayari umekamilika kwa sehemu kubwa na haijafahamika mara moja ni kwa kiasi gani hatua hiyo ya Marekani itateteresha ukamilishaji wa kipande kilichosalia.

No comments:

Post a Comment

Punguza kilo tano kwa siku saba

  NI watu wachache wanaopenda kunenepa, wengi wanapenda miili ya wastani kwa kuwa  unene si mzuri. Ukiwa mnene si tu kwamba unakaribisha m...