Search This Blog

Saturday, December 28, 2019

Mwinyi Zahera aishtaki Yanga FIFA kisa madeni


Aliyekuwa Kocha wa Yanga SC, Mwinyi Zahera ameishtaki klabu hiyo katika shirikisho la soka duniani (FIFA) kwa kucheleweshewa malipo yake.

Kwa mujibu wa kanuni alivyofuatilia, Zahera ana uhakika kuwa watamlipa mara mbili ya fedha anazodai kutokana na usumbufu aliyoupata.

Kocha huyo amesema ameshafuata taratibu zote kwani anajua pesa yake alitakiwa kulipwa mapema baada tu ya kufukuzwa.

"Yanga wanasema hawana fedha sasa tutajua, maana makocha wote waliofukuzwa wakiwemo wale wa Simba na Azam FC walilipwa fedha zao siku hiyo hiyo maana huwezi kufanya maamuzi bila kujua utatoa wapi fedha', amesema Zahera.

Ikumbukwe Mwinyi Zahera alifurushwa ndani ya Yanga kufuatia matokeo mabovu ya Kombe la Shirikisho Afrika na Ligi Kuu Tanzania Bara na nafasi yake kuchukuliwa na Mkwasa.

No comments:

Post a Comment

Punguza kilo tano kwa siku saba

  NI watu wachache wanaopenda kunenepa, wengi wanapenda miili ya wastani kwa kuwa  unene si mzuri. Ukiwa mnene si tu kwamba unakaribisha m...