Search This Blog

Wednesday, December 11, 2019

Klopp alivyowafukuzisha kazi makocha England

LIVERPOOL, ENGLAND .NDIYO hivyo, Liverpool imekuwa timu moto kwa sasa kama ilivyokuwa huko zamani. Msimu uliopita walibeba ubingwa wa Ligi ya Mabingwa Ulaya na msimu huu wameweka pengo kubwa la pointi wakiongoza kwenye msimamo wa Ligi Kuu England, pointi nane dhidi ya timu inayowafuatia kwenye ligi hiyo.

Wamekuwa bora chini ya kocha wao Mjerumani, Jurgen Klopp, ambaye amekuwa na sifa ya kipekee, ukiacha kuifanya Liverpool kutesa wapinzani wake kwenye mechi mbalimbali, lakini amekuwa hodari pia kwenye kufukuzisha kazi makocha wenzake.

Hawa hapa makocha watano walipopoteza ajira zao wakati walipokumbana na Liverpool ya Klopp kwenye Ligi Kuu England.

Francesco Guidolin - Swansea, 2016

Siku nyingi zimepita, lakini Francesco Guidolin maisha yake kwenye kikosi cha Swansea City yalikwenda kuhitimishwa kwenye mchezo dhidi ya Liverpool ya Klopp. Guidolin alikuwa salama kwenye kibarua chake, lakini mambo yalibadilika baada ya kufungwa na Liverpool nyumbani, Liberty Stadium, ambapo mabao ya Roberto Firmino na James Milner yalimfanya apoteze ajira yake.

Slaven Bilic -West Ham, 2017

Advertisement

Slaven Bilic bado amekuwa na heshima kubwa kwa mashabiki wa West Ham United licha ya mambo yake kwenda kombo alipokuwa na timu hiyo. Kwa namna fulani aliifanya timu hiyo kuwa moto, lakini kibarua chake kilikwenda kuhitimishwa baada ya mechi dhidi ya mechi yao dhidi ya Liverpool ya Klopp, ambapo kwenye mechi hiyo miongoni mwa mastaa waliofunga ni Mohamed Salah.

Slavisa Jokanovic - Fulham, 2018

Fulham walipokuwa kwenye Ligi Kuu England 2017/18 walikuwa gumzo kutokana na kikosi chake kuwa na mastaa matata kama RyanSessegnon, Aleksandar Mitrovic na Tom Cairney. Lakini, baadaye walikutana na shida kwenye safu ya mabeki kitu ambacho kiliwaponza na kushuka. Mambo yalikuwa mazito wakati walipochapwa 2-0 na Liverpool na baada ya hapo, Jokanovic akafutwa kazi.

Jose Mourinho -Man United, 2018

Jose Mourinho kwa sasa ni kocha wa Tottenham Hotspur. Lakini, kabla ya hapo, miezi 12 iliyopita alikuwa kwenye kikosi cha Manchester United, ambapo mechi yake ya mwisho kwenye kikosi hicho cha Old Trafford ilikuwa dhidi ya Liverpool ya Klopp. Mourinho baada ya kukutana na kichapo cha mabao 3-1 Anfield, Man United hawakuvumilia, wakamfuta kazi.

Marco Silva -Everton, 2019

Silva ndiye muhanga wa Klopp wa siku za karibuni. Kocha huyo kibarua chake huko Everton kiliota mbawa baada ya kukupamba na kipigo kutoka kwa Liverpool ya kocha Klopp. Katika mchezo huo wa Ligi Kuu England, uliowakutanisha mahasimu hao wa Merseyside, Everton walichapwa 5-2 na Liverpool na siku iliyofuata tu, Silva alifunguliwa mlango wa kutokea.

Let's block ads! (Why?)

No comments:

Post a Comment

Punguza kilo tano kwa siku saba

  NI watu wachache wanaopenda kunenepa, wengi wanapenda miili ya wastani kwa kuwa  unene si mzuri. Ukiwa mnene si tu kwamba unakaribisha m...