Search This Blog

Wednesday, December 11, 2019

Pep Guardiola awaambia Man City mleteni Kylian Mbappe kikosini

KOCHA wa Manchester City, Pep Guardiola amewaambia mabosi wa timu hiyo kufanya kila wanaloweza kuhakikisha Kylian Mbappe anatua Etihad msimu ujao. Staa huyo wa PSG, Mbappe anatarajia kuachana na maisha ya Paris mwakani huku Real Madrid ikipewa nafasi kubwa ya kwenda kunasa huduma yake.

Lakini, France Football linaripoti kwamba Man City nao wapo kwenye mchakato wa kumnasa mshambuliaji huyo ambapo kocha Guardiola anahitaji huduma yake kwelikweli akiamini ndiye mtu anayefaa kwenda kuchukua mikoba ya Sergio Aguero. Taarifa za kutoka Madrid zinadai kwamba rais wa Los Blancos, Florentino Perez amejiandaa kulipa Euro 300 milioni kunasa saini ya staa huyo mshindi wa Kombe la Dunia.

Mara kadhaa klabu yake imekuwa ikisisitiza kwamba nyota huyu hauzwi kwa klabu yoyote, huku Monaco alikoanzia kung’ara wakiamini kwamba ni suala la muda tu, kwani Real Madrid pia wanahitaji huduma ya supastaa huyo wa kimataifa wa Ufaransa.

Let's block ads! (Why?)

No comments:

Post a Comment

Punguza kilo tano kwa siku saba

  NI watu wachache wanaopenda kunenepa, wengi wanapenda miili ya wastani kwa kuwa  unene si mzuri. Ukiwa mnene si tu kwamba unakaribisha m...